Maahadi ya Quráni inaendelea kutoa semina kwa njia ya intanet

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya inaendesha semina ya hukumu za usomaji wa Quráni ikiwa na wanafunzi (80) kwa vipindi (12).

Masomo yamefundishwa kwa kutumia mitandao ya intanet, kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, aidha semina hii ni sehemu ya kuendeleza mafundisho ya Maahadi.

Tambua kua haya masomo ni sehemu ya harakati zinazo fanywa na Maahadi ya Quráni pamoja na matawi yake, na kuendelea kuitumikia Quráni pamoja na kuwepo kwa janga la Korona.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya imezowea kufanya harakati mbalimbali kuhusu Quráni tukufu, lakini kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia wa sasa na hatua za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona zinazochukuliwa na Atabatu Abbasiyya, mwaka huu tumetosheka na harakati chache ikiwa ni pamoja na semina hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: