Idara ya usafi inafanya kazi ya kusafisha maeneo ya Atabatu Abbasiyya tukufu masaa (24)

Maoni katika picha
Idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi inafanya kazi ya kusafisha maeneo yote yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya masaa (24) kila siku.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Faahir Zaahir Abuud ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “watumishi wa idara yetu wanasafisha maeneo yanayo zunguka Ataba kila siku, wanafagia na kupiga deki pamoja na kuondoa mabaki ya vitu, kazi hiyo wanafanya kila siku masaa (24)”.

Akaongeza kuwa: “Wanafanyia kazi maelekezo yaliyo tolewa na idara ya afya katika Ataba tukufu, wanavaa vifaa kinga na barakoa wakati wa kazi sambamba na kutumia vitakasa mikono kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Tambua kuwa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya ni miongoni mwa idara muhimu, kutokana na wajibu wake wa kuhakikisha mazingira yanayo zunguka Ataba yanakua safi muda wote.

Kumbuka kuwa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya ni miongoni mwa vitengo ambavyo vinatoa huduma ya moja kwa moja kwa zaairu, na hujitahidi kuhakikisha inatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: