Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinasaidia kutoa huduma ya matibabu kwa watu walio ambukizwa virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu Shaábi) kinasaidia idara ya afya ya mkoa wa Karbala, kutoa huduma za matibabu kwa watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Karbala wakiwa majumbani kwao.

Msemaji wa kikosi hicho ameripoti kuwa: Kamati maalum ya kupambana na maambukizi imekutana na ujembe wa idara ya afya ya mkoa wa Karbala, ambao ni Dokta Khalid Aáraji na wajumbe wawili alio fuatana nao, wakajadili mpango wa kikosi kusaidia idara ya afya ya Karbala kwa kutoa huduma za matibabu kwa watu walio ambuizwa virusi vya Korona wanao tumia dawa wakiwa majumbani kwao, pamoja na kuandaa vifaa tiba vyote vinavyo hitajika.

Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) Ustadh Maitham Zaidi amesifu kazi nzuri inayo fanywa na wahudumu wa afya katika mkoa wa Karbala na kwa namna wanavyo thamini maisha ya mwananchi.

Tambua kuwa kikosi kilikua kimesha unda kikosikazi cha kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, chenye jukumu la kupuliza dawa kwenye nyumba za makazi ya watu ndani na nje ya mji wa Karbala pamoja na mikoa mingine ya Iraq, kimefanya kila jambo linalo wezekana katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: