katika kumbukumbu ya sita.. Atabatu Abbasiyya imetumia bilioni nane (8) kwa wapiganaji wa fatwa tukufu ya kujilinda na bado inaendelea kusaidia

Maoni katika picha
Idara ya misaada na maelekezo chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya ambacho mwaka huu kina adhimisha miaka sita ya kuanzishwa kwake sambamba na kuadhimisha kumbukumbu ya kutolewa kwa fatwa ya kuilinda Iraq na maeneo matakatifu, ilikuwa miongoni mwa taasisi za kwanza kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusaidia jeshi la serikali na wapiganaji wa kujitolea pamoja na mashahidi na majeruhi, ilikua na mchango mkubwa katika vita hadi kupatikana kwa ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh na kukomboa ardhi tukufu ya Iraq, ilitoa misaada ya aina tofauti ikiwa ni pamoja na kusimama mstari wa mbele katika uwanja wa vita kusaidia wapiganaji, mashahidi na majeruhi, kiasi cha pesa iliyo tumika kusaidia kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kinakaribia bilioni nane (8) dinari za Iraq, na bado idara inaendelea kutoa misaada.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo Shekh Haidari Aaridhi, akaongeza kuwa: “Tangu ilipo tolewa fatwa ya kujilinda Atabatu Abbasiyya imekuwa mstari wa mbele katika uwanja wa vita, kupitia idara ya misaada na maelekezo, iliyo anzishwa mara tu baada ya kutolewa fatwa hiyo na Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, ikatenga pesa kwa ajili ya kusaidia mambo ya lazima kwa wapiganaji waliopo kwenye uwanja wa vita”.

Akafafanua namna pesa hizo zilivyo tumika kwa kusema kuwa: “Pesa ilitumika baada ya kufanya utafiti na kwenye maeneo yafuatayo:

  • - Kusaidia askari wa serikali na Hashdu-Shaábi kwenye uwanja wa vita, ikiwa ni pamoja kuwapa pesa za kujikimu, miwani ya usiku, nguo za kijeshi vyakula vya aina mbalimbali vikavu na vilivyo pikwa, maji pamoja na vifaa vingine.
  • - Kuwasiliana na familia za mashahidi na kuzisaidia pesa za kujikimu, familia ya shahidi hupewa pesa moja kwa moja baada ya kutembelea sehemu ya makazi yao au wao kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu au kupitia muwakilishi wa familia iwapo kutakuwa na udhuru wa kuwatembelea au wao kuja.
  • - Kuwasiliana na askari walio jeruhiwa au wapiganaji wa Hashdu-Shaábi wakiwa majumbani kwao au hospitalini pamoja na kuwapa pesa zitakazo wasaidia katika matibabu na mtihani walio nao.
  • - Kutoa posho ya pesa kwa wapiganaji wasiokua na mshahara au wanao hitaji msaada wa kibinaadamu.
  • - Kugharamia matibabu ya majeruhi au familia yake kwa kuwapeleka katika hospitali ya rufaa Alkafeel”.

Akasema: “Misaada ya idara hii haikuwalenga wapiganaji wa Hashdu-Shaábi peke yake, bali iliwahusu wapiganaji wote bila kuangalia nafasi zao hadi kikosi cha kupambana na ugaidi, pamoja na kila kikundi kilicho changia kupatikana kwa ukombozi wa Iraq, bila kuwasahau Hashdu-Shaáiriy kutoka katika miji iliyo kombolewa kutoka chini ya udhibiti wa magaidi wa Daesh, pamoja na mashahidi na majeruhuhi walio itikia wito wa Marjaa Dini mkuu na waandishi wa habari za kivita”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: