Amewasifu kuwa ni watukufu.. Marjaa Dini mkuu: kazi inayofanywa na wahudumu wa afya ni sawa na kazi inayo fanywa na askari waliopo kwenye uwanja wa vita

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesifu kazi inayo fanywa na wahudumu wa afya ya kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona, amesema kuwa hiyo ni kazi kubwa na tukufu inakaribia utukufu wa askari wanaopambana kulinda taifa lao, na amewaita kuwa ni watukufu.

Hayo yapo katika jibu la swali lililotumwa kwenye ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani mwezi (21 Rajabu 1441h) sawa na tarehe (17 Machi 2020m) kuhusu mazingira waliyonayo wahudumu wa afya wanao jitolea kuwahudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona mahospitalini na kwenye vituo vya afya, lifuatalo ni jibu alilotoa kuhusu swala hilo: (Bila shaka kazi inayo fanywa na ndugu watukufu –pamoja na changamoto zake- ni kazi kubwa isiyolinganishwa kwa thamani, tena umuhimu wake ni sawa na askari waliopo kwenye uwanja wa vita kwa ajili ya kulinda taifa lao na raia).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: