Kitengo cha usimamizi wa kihandisi: kimekamilisha hatua ya kwanza katika ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha sita kwenye mkoa wa Muthanna

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wamemaliza hatua ya kwanza katika ujenzi wa kituo cha kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona Alhayaat cha sita kwenye mkoa wa Muthanna, kinacho jengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500), hatua ya kwanza imekamilika kwa asilimia %100.

Mhandisi mkazi wa mradi huo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kwa kufanya kazi mfululizo hadi usiku, tumefanikiwa kumaliza hatua ya kwanza, hatua ya kujenga msingi kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500) chini ya vigezo tulivyo kubaliana na wanufaika”.

Akafafanua kuwa: “Sehemu iliyokua imebaki na ambayo tayali imekamilika ilikua ni ile ya lango kuu na vyumba vya madaktari na vya dawa, hivyo hatua ya kwanza ambayo ni muhimu zaidi inakua imekamilika na tutaanza kujenga boma la chuma”.

Akasema: “Tunafanya kazi saa (12) kila siku kwa ajili ya kuhakikisha tunamaliza ndani ya muda uliopangwa, miongoni mwa kazi zinazo endelea ni:

  • - Kuweka mabomba ya maji taka.
  • - Kuweka sakafu kwenye vyumba vya vyoo na kukamilisha mfumo wa maji taka.
  • - Kufunga nyaya za umeme.
  • - Kuendelea na kazi ya kukata vyumba ambayo imekamilika kwa asilimia %90”.

Kumbuka kuwa ujenzi huu unafanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, kwa ajili ya kuchangia mapambano dhidi ya virusi vya Korona, na kuongeza uwezo wa hospitali ya Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Muthanna, unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500) na kitakua na vyumba (114) vyenye ubora mkubwa na vinavyo kidhi vigezo vya kiafya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: