Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram takatifu wanaendelea na jukumu la kufanya usafi

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya usafi chini ya kitengo cha usimamizi wa haram katika Atabatu Abbasiyya wanaendelea kutekeleza wajibu wao, kwa kusafisha sehemu zote za Ataba kila siku.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Fuad Qahtwani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu wanafanya kazi ya kufagia, kupiga deki, kupuliza dawa na kila aina ya usafi ndani ya haram takatifu, saa ishirini na nne (24) kila siku”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya usafi hugawanywa sehemu mbalimbali, wanatumia vifaa maalum visivyo athiri sakafu”.

Akasema: “Watumishi wetu wanafuata maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya kuhusu nanma ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, wanavaa vifaa kinga wakati wa kazi”.

Tambua kuwa kitengo cha usimamizi wa haram kinajukumu la kusafisha na kutandika miswala ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mambo mengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: