Kikosi cha Abbasi: kinaendelea na kupuliza dawa kwenye taasisi mbalimbali mikoani

Maoni katika picha
Majemedari wa Alkafeel katika kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) wanaendelea kupuliza dawa kwenye taasisi za serikali baada ya kuombwa na idara za taasisi hizo, hivi karibuni wamepuliza dawa kwenye wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu chini ya maelekezo ya viongozi wa kikosi kuhusu kujikinga na janga la Korona.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: wawakilishi wa kikosi katika mji wa Baabil wamepuliza dawa kwenye kitengo cha mawasiliano kilicho chini ya ofisi za polisi wa mkoa wa huo katika vyumba vyote na njia zinazo zunguka eneo hilo.

Akafafanua kuwa: wawakilishi wetu waliopo Diwaniyya wamepuliza dawa kwenye maeneo yaliyo ripoti visa vya maambukizi, kama vile wilaya ya Somar, baada ya kupokea maombi kutoka kwa watumishi wa afya wa wilaya hiyo kufuatia mmoja wa wafanyakazi wa maabara kuambukizwa virusi vya Korona, ndipo wakaitikia wito na kwenda kupuliza dawa baada ya kuwasiliana na kituo cha afya.

Akaongeza kuwa: aidha wawakilishi wa kikosi cha Abbasi katika mji wa Basra waliobwa kwenda kupuliza dawa na kituo cha ukaguzi katika mkoa huo, baada ya kuambukizwa virusi vya Korona mmoja wa askari wa kituo hicho, wameenda na kupuliza dawa eneo lote la kituo.

Akasema kuwa majemedari wa kikosi chetu wanaendelea kulitumikia taifa na wananchi hadi janga hili litakapoisha kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: