Kitengo cha usimamizi wa kihandisi kimesema kuwa: ujenzi wa kituo cha Alhayaat katika mkoa wa Muthanna unaendelea.

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha uhandisi wanaojenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona Alhayaat chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya idara ya afya ya mkoa wa Muthanna, wamesema kuwa mradi umekamilika kwa zaidi ya asilimia %50, kazi inaendelea sehemu mbalimbali, tunafanya kazi kwa zaidi ya saa (12) kwa siku, kazi inaendelea kama ilivyo pangwa.

Mhandisi mkazi wa mradi Swafaa Muhammad Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kumaliza kuandaa kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500) na kuendelea na hatua zingine za ujenzi hadi sasa tumesha fikia zaidi ya asilimia %50”.

Akamongeza kuwa: “Kazi za hatua zingine zinaendelea kwa pamoja, miongoni mwa kazi hizo ni:

  • - Ujenzi wa boma la chuma umekamilika kwa asilimia %85.
  • - Kumwaga zege la msingi, kumekamilika kwa asilimi %100.
  • - Kuweka njia za mati pamoja na bomba za maji taka.
  • - Kujenga sakafu kwenye kila chumba cha choo, na kujenga mfumo wa vyoo kwa ujumla.
  • - Kujenga mfumo wa kutoa hewa chafu (AIR FRESH).
  • - Kuendelea na kazi ya kufunga nyaya za umeme.
  • - Kuendelea na kazi ya kukata vyumba ambayo imekamilika kwa asilimia %90”.

Kumbuka kuwa ujenzi huu unafanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuongeza nguvu katika mkakati wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na kuongeza uwezo wa kupokea wangonjwa katika hospitali ya Hussein (a.s) mkoani Muthanna, unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500), kitakua na vyumba (114) vyenye ubora na viwango vilivyo pasishwa na wanufaika pamoja na kukidhi vigezo vya idara ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: