Jopo la madaktari katika hospitali ya Alkafeel limefanikiwa kumtibu mtoto aliyekua na maradhi ya degedege.

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kumtibu mtoto wa miezi miwili aliyekua na maradhi ya degedege, wamesema kuwa vifaa tiba vya kisasa vimesaidia kupatikana kwa mafanikio hayo.

Daktari wa watoto katika hospitali hiyo, Dokta Sarmad Rabii amesema kuwa: “Jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu limefanikiwa kumtibu mtoto mwenye umri wa miezi miwili aliyekua na maradhi ya degedege”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya upasuaji ilichukua muda wa saa moja na tumetumia vifaa maalum vya kisasa, bila kutokea ziada yeyote”.

Akaendelea kusema: “Upasuaji huu ni sehemu ya mfululizo wa aina nyingi za upasuaji wenye mafanikio unaofanywa na hospitali ya Alkafeel, mafanikio hayo yanatokana na vifaa tiba vya kisasa tulivyo navyo”.

Akasema: “Asilimia kubwa ya upasuaji walio fanyiwa watoto ni ule ambao ulikua haufanywi na hospitali za hapa Iraq siku za nyuma”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel imekua ikijitahidi kutoa huduma bora wakati wote kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa ilivyo navyo chini ya madaktari bingwa wenye weledi na uzowefu mkubwa wa ndani na nje ya nchi, na kuifanya kutoa ushindani mkuba katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti sambamba na kupokea wagonjwa waliopo kwenye hatua mbalimbali za maradhi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: