Mkuu wa mji wa Imamu Hussein wa kitabibu katika mkoa wa Karbala amesema kuwa: Atabatu Abbasiyya tukufu ni deni kwetu kutokana na kazi kubwa waliyo fanya katika kupambana na janga la Korona.

Maoni katika picha
Kiongozi wa mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala Dokta Swabahu Husseini, ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha nne cha kutibu watu walioambukizwa virusi vya Korona, unaotekelezwa na Atabatu Abbasiyya kupitia watumishi wake wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, kama sehemu ya kusaidia idara ya afya ya mkoa, iweze kupokea na kutoa huduma kwa watu wengi zaidi walio ambukizwa virusi vya Korona, pamoja na kuongeza uwezo wa kulaza wagonjwa wengi na kutekeleza maagizo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza swala hilo.

Ugeni huo umepokelewa na rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, Mhandisi Samiir Abbasi na wasimamizi wa utekelezaji wa mradi, ametoa maelezo kwa ufupi kuhusu hatua za ujenzi wa kituo hicho ambao unakaribia kukamilika, pamoja na vifaa tiba vya kisasa vitakavyo tumika na huduma zitakazo tolewa.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi mkazi wa mradi bwana Muhammad Mustwafa Twawil aliye fuatana na ugeni huo, amesema kuwa: “Dokta Swabaah Husseini amesifu namna ujenzi unavyo endelea pamoja na changamoto zilizopo, akawashukuru watendaji wa mradi pamoja na Atabatu Abbasiyya na uongozi wake chini ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, akasema kuwa kazi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kujenga vituo hivi, katika mazingira haya magumu ambayo taifa linapitia kwa sasa, na namna wanavyo pambana na janga hili ni deni kwetu, mwisho akaomba samahani kwa kutofuatilia kwake ujenzi huu tangu mwanzo, kutokana na kushughulishwa na kusimamia matibabu ya baadhi ya watu walio ambukizwa virusi vya Korona”.

Kumbuka kuwa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha nne ni sehemu ya msaada wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa idara ya afya ya mkoa, na kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa wa Korona, kinajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1000) kimegawiwa sehemu mbili:

Sehemu ya kwanza: Inaukubwa wa mita za mraba (350) na inavyumba sita vya madaktari kila kimoja kinaukubwa wa mita za mraba (12) pamoja na maabara yenye ukubwa wa mita za mraba (24) na chumba cha mionzi, aidha kuna chumba cha utawala chenye ukubwa wa mita (24) na ukumbi wa mapokezi pamoja na vyoo sita, vitatu vya wanaume na vitatu vya wanawake, halafu kuna ukumbi wa kukaa watu wanaosubiri kuhudumiwa, eneo loto kwa ujumla lina mita za mraba (114).

Sehemu ya pili: Inaukubwa wa mita za mraba (600), inavituo (15) vilivyo gawika sehemu mbili zilizopo pande mbili za kituo, pamoja na vyumba vya wauguzi, chumba cha dawa na vyoo maalum vya wahudumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: