Maahadi ya Quráni tukufu imetangaza kuanza kwa usajili wa semina za Quráni za majira ya kiangazi

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kusajili washiriki wa semina za Quráni za majira ya kiangazi zitakazo fanywa mwaka huu kwa njia ya mtandao, kutokana na maelekezo ya wizara ya afya yanayo kataza mikusanyiko, sambamba na kufanyia kazi muongozo wa Marjaa Dini mkuu alio toa kuhusu virusi vya Korona na namna ya kujikinga navyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa Maahadi Shekh Jawadi Nasrawi “Mwaka huu mafunzo yatatolewa kwa njia ya mtandao kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa pamoja na dunia kwa ujumla ya maambukizi ya virusi vya Korona, kutokana na umuhimu wa mradi huu ambao hutekelezwa na Maahadi kila mwaka, na kuhakikisha tunaendelea kutumia vizuri kipindi cha likizo za majira ya kiangazi kwa kuzilea nafsi kupitia masomo ya (Quráni, Aqida, Fiqhi, Akhlaq, na Sira)”.

Shekh Nasrawi akasema: Idara ya Maahadi imeweka masharti ya kujiunga, ambayo ni:

  • 1- Ushiriki ni kwa wavulana pekeyake.
  • 2- Asiwe chini ya miaka (6) na asizidi miaka (15).
  • 3- Awe na simu yenye Telegram.
  • 4- Ajisajili kwa kujaza fomu kwa njia ya mtandao kwenye link ifuatayo: net/quran/register.php?i=1
  • 5- Namba ya simu atakayo weka kwenye fomu iandikwe kwa lugha ya Kiingereza.

Akamaliza kwa kusema: “Baada ya kukamilisha usajili siku ya Jumanne (14/07/2020m) na kubaini majina ya washiriki kutoka ndani na nje ya Iraq, tutatoa malekezo ya namna ya kushiriki kwenye mafunzo”.

Kumbuka kuwa mradi wa semina za Quráni za majira ya kiangazi ni mradi muhimu katika Maahadi ya Quráni tukufu, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya unatoa kipaombole kikubwa kwa mradi huo, kutokana na umuhimu wa malezi sahihi kwa kizazi hiki yanayo patikana kwenye mradi huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: