Jengo la kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona Alhayaat la nne katika mkoa wa Karbala lipo katika hatua za mwisho

Maoni katika picha
Kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kuwa mafundi wake wanaofanya kazi katika mradi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s), kinacho jengwa ili kusaidia sekta ya afya kupambana na janga hilo, wapo katika hatua ya mwisho ya awamu ya tano, siku chache zijazo jengo hilo litakabidhiwa kwa idara ya afya ya Karbala, likiwa limekamilisha vigezo vyote vya afya, litakuwa msaada mkubwa katika sekta ya afya ukizingatia kuwa litaongeza uwezo wa kulaza wagonjwa, na kupokea wagonjwa wengi jambo hilo litasaidia kupunguza mzigo kwenye vituo vingine.

Haya yameelezwa na Mhandisi mkazi wa mradi bwana Muhammad Mustwafa Twawil, akaongeza kusema kuwa: “Hatua ya umaliziaji katika kila mradi hua ni hatua muhimu, hususan katika miradi ya kiafya, watumishi wetu wanafanya kazi kubwa katika hatua hii na zilizo pita, wanataka kukamilisha mradi ndani ya muda uliopangwa pamoja na changamoto za uchache wa watumishi, ukizingatia kuwa kitengo hiki kinajenga vituo vingine vya aina hii katika mkoa wa Bagdad na Muthanna, pamoja na kazi zingine za Ataba tukufu na kuongezeka kwa kiwango cha joto, bila kusahau ukaribu wa eneo hili na sehemu wanapo hudumiwa watu walio ambukizwa virusi vya Korona, lakini changamoto zote hizo zimekua chachu ya kuhakikisha wanamaliza kazi kwa wakati”.

Akaongeza kuwa: “Kazi inayo endelea kwa sasa ni umaliziaji, pamoja na ufungaji wa njia za maji safi na maji taka, sambamba na kufunga mitambo ya kuingiza hewa safi vyumbani, pamoja na kuunganisha umeme kutoka kituo kikuu cha umeme wa taifa cha hapa Karbala, na kuweka vipande vya mbao kwenye sehemu za njia kama sehemu za urembo na kuandaa sakafu kwa ajili ya kuweka ruva”.

Akamaliza kwa kusema: “Mafundi wanamalizia matengenezo kwenye vyumba vyote vya wagonjwa, na kuweka vifaa tiba na vifaa vya kiofisi”.

Kumbuka kuwa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha nne ni sehemu ya msaada wa Atabatu Abbasiyya kwa idara ya afya ya mkoa wa Karbala wa kuongeza uwezo wa kulaza wagonjwa wa Korona, kinajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (1000) umegawika sehemu mbili:

Sehemu ya kwanza: Inaukubwa wa mita za mraba (350) na inavyumba sita vya madaktari kila kimoja kinaukubwa wa mita za mraba (12) pamoja na maabara yenye ukubwa wa mita (24) na chumba cha mionzi, aidha kuna chumba cha utawala chenye ukubwa wa mita (24) na ukumbi wa mapokezi pamoja na vyoo sita, vitatu vya wanaume na vitatu vya wanawake, halafu kuna ukumbi wa kukaa watu wanaosubiri kuhudumiwa, eneo loto kwa ujumla lina mita za mraba (114).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: