Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umekutana na mkuu wa mkoa wa Karbala na kujadili ujenzi wa barabara ya Jamhuriyya chini ya mtazamo wa uhandisi wa kiislam

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar amefanya mkutano muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Khatwabi, na marais wa idara za utumishi za mkoa, idara ya majengo, maji, umeme na mkuu wa mipangomiji, upande wapili walikuwa ni wajumbe wa idara kuu ya uongozi katika Ataba tukufu pamoja na baadhi ya marais wa vitengo vya Ataba.

Katika kikoa hicho wamejadili ujenzi wa barabara ya Jamhuriyya inayo onganisha daraja la Babu-Towareg na Babu-Qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kujiandaa na ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu pamoja na matembezi ya Towareg ambayo hufanywa mwezi kumi Muharam pamoja na kupaka rangi kwenye barabara inayo endana na utukufu wa mji wa Karbala.

Kuhusu swala hilo; katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuendeleza mji mtukufu wa Karbala, tumefanya kikao muhimu na mkuu wa mkoa wa Karbala pamoja na idara za utendaji, tumejadili kuhusu kuboresha barabara ya Jamhuriyya ili iendano na utukufu wa mji huu, pamoja na kuweka mambo yote muhimu katika kumuhudumia zaairu wakati wa ziara ya mwezi kumi Muharam na ziara ya Arubaini pamoja na ziara zingine”.

Naye mkuu wa mkoa wa Karbala Mhandisi Naswifu Jaasim Khatwabi akasema kuwa: “Tumekutana na viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wakiongozwa na katibu mkuu wa Ataba hiyo Mhandisi Muhammad Ashiqar na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na baadhi ya marais wa vitengo vya Ataba, tumejadili wazo la kiongozi mkuu wa kisheria kuhusu kuboresha mji mtukufu wa Karbala, jambo la kufurahisha ni kwamba Sayyid Ahmadi Swafi alizungumzia umuhimu wa kuuendeleza mji wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Kikao kilikuwa muhimu sana kwani tumejadili namna ya kuboresha barabara ya Jamhuriyya iliyopo katikati ya mji wa Karbala, nayo ni barabara muhimu hasa wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu kila mwaka, misafara mingi ya mazuwaru hutumia barabara hiyo yakiwemo matembezi ya Towareg ambayo hufanywa mwezi kumi Muharam katika kumbukumbu ya kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s), aidha barabara hiyo ni muhimu katika upande wa uchumi kwa wakazi wa Karbala, ni muhimu kuboreshwa barabara hiyo ambayo ni kielelezo cha utamaduni wa mji wa Karbala”.

Akafafanua kuwa: “Tumezungumzia vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kuunda kamati maalum itakayo husika na kuandaa mapendekezo ya kihandisi kuhusu namna ya kuboresha barabara hiyo, kamati hiyo inatakiwa kuwasilisha mapendekezo yao haraka iwezekanavyo, na kuweka vipaombele vya kiutendaji”.

Akasema: “Mkakati umegawanywa sehemu mbili, kwanza ni mpango kazi pamoja na makadirio ya muda, na sehemu ya pili ni utendaji wa kazi, na kuhakikisha inakamilika kabla ya mwezi kumi Muharam mwaka huu, iwe tayali imesha ongezwa pamoja na kumaliza ukarabati mwingine kabla ya ziara ya Arubaini ya mwaka huu”.

Baada ya kumaliza majadiliano wajumbe wote walielekea katika mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kukubaliana vipengele vya kuanza navyo katika ujenzi wa barabara ya Jamhuriyya na barabara ya Babu-Qibla, halafu wakaenda katika soko la (Alawiy) kuangalia namna ya kuliboresha katika mpango kazi utakao anza kutekelezwa hivi karibuni Insha-Allah.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: