Makumi ya mahafidh wamehitimu kwa walimu wa idara ya tahfiidh katika Maahadi ya Quráni tukufu

Maoni katika picha
Kazi kubwa inafanywa na idara ya tahfiidh chini ya Maahadi ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya tukufu ya kufundisha utamaduni wa kufuata mafundisho ya Quráni, imechukua jukumu la kuhifadhisha Quráni tukufu.

Kuhusu utendaji kazi wa idara hii tumeongea na Ustadh Mustwafa Sa’duni mmoja wa wahadhiri wa idara hiyo, amesema kuwa: Idara yetu imechukua jukumu la kuhifadhisha Quráni chini ya walimu walio bobea kwenye fani hiyo.

Akasema: Tumeanza tangu miaka sita (6) iliyo pita, ndani ya kipindi hicho tumefaulisha makumi ya mahafidh wa Quráni nzima na wengine walio hifadhi majuzuu kadhaa huku wakisoma kwa ufasaha na kufuata hukumu za usomaji.

Akaendelea kusema: wanafunzi wetu wameshiriki kwenye mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Sa’duni akaendelea kusema: miongoni mwa miradi muhimu iliyo fanywa na idara ya tahfiidh ni mradi wa Haafidh Maahir, nao ni mradi mkubwa uliofanywa na Maahadi unaolenga kuendeleza uwezo wa mahafidh.

Miongoni mwa harakati muhimu zinazo fanywa kila mwaka ni usomaji wa Quráni kwa hifdhu ndani ya mwezi wa Ramadhani.

Mwisho wa mazungumzo yeke Sa’duni akafafanua kuwa: Idara bado inaendelea kufundisha kwa kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona na kufuata maelekezo ya wizara ya afya.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imezowea kufanya harakati mbalimbali za Quráni kila mwaka, lakini kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa na hatua za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona zinazo chukuliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, mwaka huu tumetosheka na harakati chache ikiwemo hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: