Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wameanza kufunga (Jipsam-bord) kwenye jengo la Alhayaat la sita katika mkoa wa Muthanna

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, wanaojenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona Alhayaat cha sita, kazi inayo endelea hivi sasa katika hospitali ya Hissein (a.s) ambayo ipo chini ya idara ya afya ya mkoa wa Muthanna, wameanza kuweka (PVC) kwenye vyumba (114) sambamba na kufunga (Jipsam-Bord).

Mhandisi mkazi wa mradi huo bwana Swafaa Muhammad Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kumaliza kazi ya kukata vyumba kwa kutumia (Sandwich-panel) tumeanza kazi za umaliziaji ikiwa ni pamoja na kufunga (Jipsam-Bord) na kuweka madirisha”.

Akabainisha kuwa: “Hali kadhalika tumeanza kuweka lami kwenye uwanja wa kituo pamoja na ruva sambamba na kufunga bomba za mazi”.

Akafafanua: “Tunafanya kazi hizi baada ya kumaliza sehemu ya nne na ya mwisho ya ujenzi wa vyumba vya madaktari na wauguzi, pamoja na kuendelea kufunga mitambo ya kuingiza hewa safi (AIR FRESH) na kufunga nyaya za umeme”.

Kumbuka kuwa ujenzi wa kituo hiki unaofanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, unafanywa kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Korona, na kuongeza uwezo wa kupokea wagonjwa katika hospitali ya Hussein (a.s) iliyopo mkoani Muthanna, kinajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (3500) na kitakuwa na vyumba (114) vilivyo kamilisha vigezo vyote tulivyo kubaliana na wanufaika sambamba na kukidhi masharti ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: