Chapisho la jarida la nane la (Turathi za Basra).

Maoni katika picha
Katika muendeleza wa machapisho yanayo andika turathi za mkoa wa Basra na kuonyesha hazina zake, hivi karibuni kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimetoa chapisho la jarida la (Turathi za Basra).

Jarida hilo limejaa tafiti nyingi za kielimu, miongoni mwa tafiti hizo ni:

  • - Utafiti kuhusu historia ya Abu Yahya Saaji na kuonyesha mchango wake wa kielimu.
  • - Utafiti usemao: (Utangulizi wa harakati ya Husseiniyya katika vitabu vya Basra).
  • - Utafiti usemao: (Juhudi za wasomi wa nahau wa Basra katika kitabu cha Sherehe ya Ibun Aqiil).
  • - Kuangalia mchango wa wasomi wa Basra kwenye masomo tofauti kupitia utafiti usemao: (Mchango wa wanachuoni wa Basra katika elimu ya Dini huko Andalusi).

Pamoja na tafiti zingine kuhusu turathi za Basra chini ya kanuni maalum za kielimu.

Kumbuka kuwa jarida la turathi za Basra ni moja ya majarida yanayo tolewa na kituo, nalo hujikita katika kuandika turathi za mji huu pamoja na baadhi ya maeneo ya kihistoria.

Tunapenda kukufahamisha kuwa unaweza kuangalia machapisho na harakati za kituo kupitia toghuti ya kituo ifuatayo (https://mk.iq).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: