Waziri wa vijana na michezo amesema kuwa: Miradi ya Ataba tukufu inasifa nzuri kutokana na uaminifu wa watendaji wake

Maoni katika picha
Waziri wa vijana na michezo bwana Adnani Darjali amesema kuwa miradi ya Ataba tukufu imepata sifa nzuri kutokana na uaminifu wa watendaji wake, jambo hilo tumeliona tulipo tumbelea Atabatu Abbasiyya hivi karibuni.

Waziri ameyasema hayo baada ya kumpokea kwenye ofisi yake Ustadh Muhammad Ali Taajir Mkuu wa kituo cha masoko na matangazo Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya, akaongeza kusema kuwa: “Baada ya ziara yetu ya mwisho tunategemea kufanyiwa kazi mambo tuliyo kubaliana ya kuwatumikia vijana na kukuza vipaji vyao”.

Naye mkuu wa kituo cha masoko Alkafeel akatoa maelezo kwa ufupi kuhusu kazi zinazo fanywa na kituo hicho, pamoja na miradi mingine inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya.

Baada ya mazungumzo yao waziri akapewa mwaliko wa kutembelea tena miradi ya Ataba tukufu, amekubali mwaliko huo na akaahidi kutembelea haraka iwezekanavyo, ametanguliza shukrani za dhati kwa kupewa mwaliko huo na akasema utasaidia kuandaa mipango kazi ya vijana, na kunufaika na uzowefu wa Ataba tukufu kwenye sekta ya viwanda na kilimo, na kutengeneza mazingira mazuri kwa vijana na wahitimu kwa ajili ya kujenga mustakbali wao na kuimarisha uchumi wa taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: