Pamoja na kupungua kidogo hatari ya maambukizi: kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili takatifu kinafanya opresheni kubwa ya usafi na kupuliza dawa

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu kinasafisha na kupuliza dawa kwenye eneo hilo na katika barabara zinazo elekea kwenye haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kwenye barabara za pembezoni mwake na kwenye majengo yote yakutolea huduma, sambamba na kuanza kupunguzwa kidogo kidogo kwa tahadhari za kujikinga.

Hayo yamesemwa na rais wa kitengo hicho Sayyid Nafii Mussawiy, akaongeza kusema kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu wamezowea kufanya usafi mfululizo pamoja na kupuliza dawa kila wakati kwa kufuata ratiba maalum iliyopo”.

Akaendelea kusema: “Idara ya usafi imeshiriki kwenye opresheni hii, baada ya kumaliza kufanya usafi wamepuliza dawa ya kujikinga na maambuizi ya virusi vya Korona kwa ajili ya kuwalinda mazuwaru na watumishi, sambamba na kuzingatia maagizo ya Atabatu Abbasiyya na kamati inayo fuatilia swala hilo”.

Akamaliza kwa kusema: “Kutokana na maelekezo ya idara ya afya katika Atabatu Abbasiyya, tumechukua tahadhari zote za kuwakinga na maambukizi watumishi wa kitengo chetu na kuhakikisha usalama wao, tumepunguza idadi ya watumishi kwenye kila zam, pamoja na kuwapulizia dawa kila wanapo maliza kazi”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imechukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya vurusi vya Korona na inafanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya katika ngazi ya Ataba, mji mkongwe na mkoa wote kwa ujumla, kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili kina nafasi kubwa katika kutekeleza baadhi ya majukumu hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: