Kituo hiki kimejikita katika kutafiti mambo ya kiutamaduni na historia ya turathi za mji wa Karbala, miongoni mwa mafanikio yaliyo patikana ni:
- - Kutoa makumi ya machapisho kuhusu turathi likiwemo jarida la (Mausua turathi Karbala).
- - Kuendesha nadwa, makongamano na maonyesho ya turathi.
- - Kukusanya kila kinacho weza kukusanywa miongoni mwa turathi za Karbala.
- - Kimekuwa mstari wa mbele katika kuibua turathi mbalimbali na bado watumishi wake wanaendelea na kazi hiyo.
Kituo kina machapisho yafuatayo:
- - Jarida la turathi za Karbala: nalo huandika tafiti mbalimbali za kielimu.
- - Jarida la turathi za Karbala za kimaandishi: nalo huandika tafiti kuhusu turathi za nakala-kale za Karbala.
- - Jarida la Ghadhwiriyya: nalo huandika malikale za Karbala.
Kituo kina idara zifuatazo:
- - Idara ya faharasi ya nakala-kale.
- - Idara ya uhakiki.
- - Idara ya habari.
- - Idara ya mawasiliano na ufuatiliaji.
- - Idara ya watumishi.
Tambua kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya pamoja na kuwa na kituo cha turathi za Karbala, kinavituo vingine viwili, ambavyo ni kituo cha turathi za Hilla na kituo cha turathi za Basra.