Toleo la nne la mausua ndogo ya Basra

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimetoa chapisho la nne la (Mausua ndogo ya Basra) lenye anuani isemayo (Harakati za Dini katika kisiwa cha Basra na wanachuoni wake (mwaka 844 – 1078h / 1440 – 1667m), linaangazia mchango wa mji wa Basra katika elimu ya Dini.

Toleo hili limeandika turathi za kielimu za wanachuoni wa Basra kwa kuzingatia wakati na maudhui, pamoja na kubainisha mwenendo wao na uhusiano wao na shule za kidini ndani na nje ya Basra, jarida hili limeandika familia nyingi zilizo julikana katika uwanja wa elimu kwa kuandika vitabu ambavyo vimekuwa vikifundishwa vyuoni, pamoja na kuangazia siasa zilizokuwepo wakati huo, na kubainisha athari yake katika harakati za Dini.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Basra huchapisha majarida mbalimbali kuhusu turathi za Basra za kidini na kihistoria.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: