Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wameanza kazi ya kufunga viyoyozi kwenye kituo cha Alhayaat cha sita katika mkoa wa Muthanna

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaojenga kituo cha Alhayaat cha sita kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, ujenzi unao endelea hivi sasa katika hospitali ya Hussein (a.s) ili kusaidia sekta ya afya katika mkoa wa Muthanna, wameanza kufunga viyoyozi kwenye vyumba (114) sambamba na kufunga mfumo wa kuingiza hewa safi (AIR FRESH).

Mhandisi mkazi wa mradi huo bwana Swafaa Muhammad Ali amesema kuwa: “Mafundi na wahandisi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wanaanza kazi asubuhi sana na wanamaliza usiku kila siku bila kupumzika, miongoni mwa kazi wanazo fanya ni:

 • - Kuweka madirisha (PVC).
 • - Kuweka (Jipsam-bord).
 • - Kufunga dari.
 • - Kufunga vipande vya (PVC) kwenye vyumba (114).
 • - Kuweka mfumo wa mati taka kwenye vyoo vya vyumbani.
 • - Kufunga mfumo wa maji safi kwenye kila chumba.
 • - Kufunga mfumo wa zimamoto.
 • - Kuweka marumaru kwenye kila chumba cha choo.
 • - Kufunga mfumo wa kuingiza hewa safi (AIR FRESH).
 • - Kuendelea na kazi ya kufunga nyaya za umeme.
 • - Kuendelea na kazi ya kukata vyumba ambayo imesha kamilika kwa zaidi ya asilimia (%90).
 • - Kuweka vipande vya zege kwenye sehemu zinazo tenganisha kati ya jengo na sehemu zilizo wekwa lami.
 • - Ujenzi wa boma la chuma umekamilika kwa asilimia %100.
 • - Ujenzi wa msingi umekamilika kwa asilimia %100.

Kumbuka kuwa ujenzi huu unafanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni sehemu ya kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Korona, na kuongeza uwezo wa hospitali ya Hussein (a.s) katika mkoa wa Muthanna, unajengwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (3500), kutakua na vyumba (114) vinavyo kidhi vigezo tulivyo kubaliana na upande wa wanufaika pamoja na vigezo vya kidaktari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: