Maktaba ya chuo kikuu cha Al-Ameed imemaliza hatua ya kwanza ya kupokea kazi za wanafunzi wa elimu ya juu waliopo nje ya Iraq

Maoni katika picha
Katika hatua nzuri kwa taifa na kuhifadhi turathi za kielimu kwa wanafunzi wa Iraq waliopo nje ya taifa, chini ya ushirikiano wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Al-Ameed na walimu wao pamoja na wanafunzi waliopo nje ya taifa, maktaba ya chuo kikuu cha Al-Ameed kwa kushirikiana na maktaba ya Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya, wamemaliza hatua ya kwanza ya kupokea kazi za wanafunzi wa elimu ya juu waliopo nje ya taifa.

Mku wa maktaba katika chuo kikuu cha Al-Ameed Ustadh Wasim Twalib amesema kuwa: “Idara inayo hudumia wanufaika kwa kushirikiana na idara ya kupangilia kazi za kielektonik wamemaliza hatua ya kwanza ya kupokea kazi hizo, kisha wamezituma kwenye kituo cha faharasi na mpangilio wa taaluma chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya, kwa ajili ya kuzitoa kwenye umbo la karatasi na kuziweka kwenye mtandao kisha kuzirudisha kwenye maktaba, hatua ya tatu itafanywa kwa kutumia program ya kisasa ya faharasi (program ya semofuni) inayo tumiwa na ofisi ya Kongresi ya Marekani, ili wanufaika waazime kwa njia ya mtandao, hususan katika mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya janga la virusi vya Korona, ndio sababu ya kuchelewa kukamilika hadi sasa, siku zijazo tutakamilisha hatua nyingine ya fani zingine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: