Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma kimepanga kufanya warsha kwa njia ya mtandao kuhusu (Faharasi na uhakiki wa nakala-kale za kiarabu)

Maoni katika picha
Kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na jumuiya ya Al-Ameed pamoja na chuo kikuu cha Al-Ameed na Alkafeel, wamekusudia kufanya warsha kuhusu (Faharasi na uhakiki wa nakala-kale za kiarabu) kupitia jukwaa la (Webinar) program ya (ZOOM Cloud Meetings) siku ya Jumatatu tarehe (13 Julai 2020) saa kumi na moja jioni.

Wakufunzi wa warsha hiyo ni:

  • - Walidi Ghali/ mkuu wa maktaba ya Aghakani huko Landan na mwalimu wa masomo ya kiarabu na kiislamu katika Maahadi ya Hadwaratu-Islamiyya.
  • - Ali Twalib/ mtaalamu wa faharasi za nakala-kale katika kituo cha faharasi na kupangilia taaluma.

Washiriki wa warsha hiyo watatunukiwa vyeti kupitia barua pepe zao, link ya kujiunga na warsha ni: https://us02web.zoom.us/webinar/register/WN__8LV_sF8QGCaAddUYsnmzA
kumbuka kuwa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, bado kinaendelea kuratibu harakati zake kwa njia ya mtandao, kama sehemu ya kutekeleza maagizo ya wizara ya afya katika kipindi hiki cha janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: