Kituo cha kuhuisha turathi kilichukua jukumu la kukihakiki, na kituo cha Shekh Tusi pia kilihakiki na kuweka anuani.
Kitabu kina juzuu tatu:
- - Juzuu la kwanza linakurasa (600) limeandika anayewajibikiwa na zaka pamoja na vitu vinavyo takiwa kutolewa zaka na vinavyo suniwa zaka, pamoja na maelezo ya zaka za wanyama na masharti ya wajibu wa zaka ya wanyama.
- - Juzuu la pili linakurasa (740) limeandika zakaa ya thamani mbili (dhahabu ba fedha) na masharti yake, kisha zaka ya nafaka nne na masharti yake halafui ikaelezewa zaka ya mali za biashara, kisha ikabainishwa namna ya kugawa zaka na wanaostahiki kupewa.
- - Juzuu la tatu linakurasa (474), limeandika sifa za wastahiki na hukumu za zaka ya mali.
Baada ya milango hiyo ukafuata mlango wa Zakatul-Fitri, jambo la kwanza kwenye mlango huo ni ufafanuzi wa nani anawajibu wa kutoa Zakatul-Fitri, anayetakiwa kupewa, aina ya vitu vinavyo takiwa kutolewa, wakati wa kutoa, kiwango cha kutoa na mwisho namna ya kugawa Zakatul-Fitri.