Kwa mara ya kwanza nchini Iraq: Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha mradi wa kufuga kware na inaingiza sokoni kware elfu mbili kila siku

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya inamiradi mingi ya viwanda, kilimo na ufugaji inayo changia pato la taifa, na kupunguza uagizaji wa bidhaa nje ya taifa, miongoni mwa miradi ambayo imeonyesha mafanikio ni mradi wa ufugaji wa kware ambao upo chini ya shirika la biashara Alkafeel, ndani ya muda mfupi wamefanikiwa kuingiza sokoni zaidi ya kware (2000) kwa siku, huu ni mradi wa kwanza hapa Iraq.

Msimamizi wa mradi huo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mradi huu umeanzishwa kwa ajili ya kupunguza uagizaji wa nyama za kware nje ya nchi, ukizingatia uzuri wa nyama hizo, hazina kiwango kikubwa cha mafuta na zinakiwango kidogo cha koresto, zinakiwango kizuri cha protini, kutokana na sifa hizo na zinginezo nyama za ndege hao zinapendwa sana, pamoja na mayai yake ambayo yanafaida kubwa tofauti na mawai mengine”.

Akaongeza kuwa: “Katika ufugaji wa ndege hao tumetumia njia za kisasa, nyama tunazo ingiza sokoni zinaubora mkubwa kwa afya ya mwanaadamu, kware wanafugwa kwenye mazingira mazuri, mayai yanatunzwa vizuri, wanakuwa hadi kufikia umri wa kuchinywa wakiwa katika hali nzuri kabisa”.

Naye Ustadh Ahmad Twalib Abdulhussein meneja masoko amesema kuwa: “Kuna mwitikio mkubwa wa bidhaa zetu, nyama na mayai, watu wameanza kutambua uzuri wa nyama za ndege hawa na faida yake katika afya zao, hivyo tumekuwa na idadi kubwa ya oda, bidhaa hizo (nyama na mayai ya kware) zinapatikana kwenye vituo vya mauzo mubashara ya shirika la biashara la Alkafeel”.

Kumbuka kuwa mradi unatekelezwa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (10,000), barabara ya (Najafu – Karbala), kuna jengo la ghorofa nne la ufugaji darasa wa kware pamoja na mashine za kutotolesha mayai na sehemu ya vifaranga, tunazalisha tani moja ya nyama za kware kila siku, hadi sasa tunazaidi ya kware elfu (30) na zinaendelea kuongezeka kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: