Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kinaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika mkoa wa Najafu

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) kinafanya opresheni kubwa ya kupuliza dawa katika mkoa wa Najafu, wanatumia vifaa vya kisasa vyenye ubora mkubwa wa kupambana na virusi vya Korona, vinavyo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hii ni sehemu ya opresheni nyingi zinazo fanywa na kikosi cha Abbasi kwenye mikoa tofauti ya Iraq, zilianza mara tu baada ya kuibuka maambukizi ya virusi vya Korona, kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu na kusaidia sekta ya afya katika mapambano dhidi ya virisi hivyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya muwakilishi wa kikosi cha Abbasi katika mkoa wa Najafu Karim Hassan, amesema kuwa: “Katika vita ya kupambana na janga la Korona na kuwatumikia wananchi wa mji wa Imamu Ali (a.s), majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) wameanza kupuliza dawa katika mkoa wa Najafu, kwa kutumia vifaa vya kisasa vilivyo andaliwa kwa ajili ya kazi hii, tumeanza kwenye mji wa zamani na mitaa yake, pamoja na kupuliza kwenye nyumba ambazo ziliripoti visa vya maambukizi”.

Naye muwakilishi wa kikosi cha Abbasi akasema kuwa: “Kiwango cha dawa iliyo tumika kwenye opresheni hiyo kimefika lita elfu hamsini, ilitengenezwa na shirika la Khairul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi ya kupuliza dawa itaendelea kwenye mkoa wa Najafu na mikoa mingine”.

Kumbuka kuwa kazi hii ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kufuata maelekezo ya idara ya afya katika kupambana na janga hili la Korona, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimekuwa mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya virusi hivyo na kinafanya kila kiwezalo kuwalinda wananchi na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: