Kituo cha turathi za Karbala kinaangazia moja ya athari za mwanachuoni wa karne ya kumi na tatu

Maoni katika picha
Miongoni mwa machapisho ya turathi yanayo lenga kuhuisha athari za kielimu za wanachuoni na watafiti, hivi karibuni kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimechapisha kitabu cha (Ujembe wa kukanusha hoja ya dhanna), kinacho tokana na uandishi wa Shekh Muhammad Taqi Harwi Haairiy mwaka (1217 – 1299h) katika wanachuoni wa karne ya kumi na tatu, kimehakikiwa na Shekh Muhammad Jafari Islami, na kituo cha turathi za Karbala kimekirejea na kuweka faharasi.

Kitabu kinakurasa (337), kimeandika hoja nyingi kuhusu dhana, pamoja na kufafanua dhana mbaya na njema, kitabu kinasehemu tatu, utangulizi, maudhui na hitimisho.

Ni wazi kuwa muandishi hakushikamana na mtazamo wa madhehebu yake kutokana na kukosekana kwa hoja ya moja kwa moja, bali asilimia kubwa ametaja udhaifu wa wanaokataa hoja za dhana kwa dalili ya msemaji, na hoja ya dhana makhsusu kama kawaida ya wahakiki.

Tambua kuwa kituo cha turathi za Karbala huchapisha majarida, vitabu na mausua, pamoja na Makala za turathi za Karbala zilizo fanyiwa utafiti na uhakiki, kama sehemu ya kuingiza habari za turathi katika maktaba za kiarabu na kiislamu pamoja na kuonyesha nafasi ya mji wa Karbala.

Kumbuka kuwa Shekh Muhammad Taqi bun Hassan Ali bun Ridhwa bun Ismail Harwi Isfahani Haairiy aliye ishi mwaka (1217 – 1299h), ni mwana chuoni mkubwa wa Dini, alikuwa mkufunzi wa Fiqhi na Usulu wa Alamah Shekh Muhammad Taqi Isfahani muandishi wa hashia ya Al-Maálim, na Haaji Muhammad Ibrahim Alkarbasi aliye andika kitabu cha Al-Isharaat, na Haaji Sayyid Muhammad Baaqir Hujjatu-Islami Rushta Isfahani. Alitembelea Iraq mara nyingi, na alihudhuria darsa la muandishi wa kitabu cha Aljawahiri katika mji wa Najafu, na huko Karbala akahudhuria darsa la Sayyid Kadhim Rushti na Mirza Ali Naqi Twabatwabai.

Kwa ajili ya kuangalia vitabu hivi na vingine vilivyo andikwa na kituo tembelea duka la vitabu lililopo karibu na mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), au katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu au fungua toghuti ifuatayo: http://www.mk.iq/cen.php?id=1
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: