Mkuu wa mkoa wa Karbala amesema kuwa: Atabatu Abbasiyya tukufu imesaidia kwa kiwango kikubwa sekta ya afya katika mkoa huu

Maoni katika picha
Mkuu wa mkoa wa Karbala Ustadh Jaasim Khatwabi amesema kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesaidia kwa kiwango kikubwa sekta ya afya katika mkoa wa Karbala hasa wakati huu wa janga la Korona, imekuwa mstari wa mbele wakati wote kusaidia watumishi wa afya, na hili sio jambo geni kwake.

Ameyasema hayo alipo hudhuria hafla ya ufunguzi wa kituo cha Alhayaat cha nne kilicho jengwa kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, alasiri ya Jumapili ya mwezi (20 Dhulqaada 1441h) sawa na tarehe (12 Julai 2020h), kilicho jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kwenye mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu.

Akaongeza kusema kuwa: “Hili ni moja ya mambo mengi yanayo fanywa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, tunaishukuru sana pamoja na kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na katibu wake mkuu pamoja na wafanyakazi wote hususan walio husika na mradi huu”.

Akamaliza kwa kusema kuwa: “Bila shaka jengo hili litasaidia kuongeza idadi ya vitanda vya wagonjwa wa Korona, kwani linavyumba maalum vya wagonjwa hao vilivyo wekwa vifaa vyote vinavyo hitajika”.

Kumbuka kuwa kukamilika kwa jengo hili kumetokana na kufanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu, aliye himiza kusaidia sekta ya afya, aidha ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kuwalinda wananchi na maambukizi ya virusi vya Korona, pia ni muongozo wa moja kwa moja kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), aliye elekeza kujenga vituo vya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona ndani na nje ya mkoa wa Karbala, hivi sasa ujenzi unaendelea kwenye vituo vingine vitatu vyenye ukubwa tofauti, kwenye mkoa wa Baabil, Bagdad na Muthanna.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: