Akiwa na umri wa miaka (8).. amerudishiwa usikivu wake katika hospitali ya rufaa Alkafeel

Maoni katika picha
Jopo la madaktari bingwa wa pua, sikio na koo katika hospitali ya rufaa Alkafeel mjini Karbala wamefanikiwa kumtibu mtoto mwenye umri wa miaka nane aliyekua na tatizo la kupoteza uwezo wa kusikia pamoja na kupumua kwa shida huku akiunguruma mfululizo usiku na mchana pamoja na kushindwa kulala.

Daktari Aadil Masudi alipo ongea na waandishi wa habari amesema kuwa, jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu limefanikiwa kumtibu mtoto mwenye umri wa miaka nane chini ya uangalizi maalum kutokana na hali yake.

Akabainisha kuwa: “Baada ya kumfanyia vipimo tuligundua kuwa, alikuwa ameota kinyama kuanzia puani hadi mdomoni ndio sababu ya kufunga mrija wa juu ya mdomo (njia ya Oksijen) pamoja na kujaa uchafu kama gundi ndani ya tundu la sikio”.

Akasema kuwa: “Hali hiyo ni ngumu sana kuamiliana nayo kwa vifaa tiba kwa kawaida, kilicho tupa ujasiri wa kufanya upasuaji huu ni ubora wa vifaa tiba vilivyopo katika hospitali ya Alkafeel ikiwemo miwani maalum na maikroskop ya kisasa, vifaa hivyo vimetuwezesha kuona ndani ya sikio na kuondoa nyama iliyokuwa imeota”.

Akaongeza kusema kuwa: “Tumeondoa uchafu uliokuwa umeganda kama gundi na kumuwekea kifaa ambacho kitatolewa baada ya muda mfupi”.

Akasisitiza kuwa: “Mgonjwa yupo katika hali ya kawaida anasikia na kupumua vizuri baada ya saa chache za kufanyiwa upasuaji”.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa maradhi tofauti kila wakati, na hupokea wagonjwa wa aina zote waliopo katika hali mbalimbali za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: