Wizara ya mawasiliano imesema kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kinatoa huduma nzuri kila sekta, lazima tusimame pamoja kuongeza uwezo wake.
Muwakilishi wa waziri Dokta Karim Muzál pembezoni mwa ziara hiyo akasema kuwa, amekutana na mkuu wa kikosi cha Abbasi Ustadh Maitham Zaidi, na kujadiliana nae kuhusu sekta ya mawasiliano, ukizingatia kuwa kikosi cha Abbasi kinamajukumu mengi ikiwa ni pamoja na kupigana, kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi na mengineyo, aidha kipo kwenye maeneo mengi ya Karbala na Iraq kwa ujumla.
Akasisitiza kuwa: “Kikosi kinatoa huduma nzuri, sisi kama wizara ya mawasiliano lazima tutoe ushirikiano kadri tuwezavyo kwa kikosi hicho, ili kuongeza uwezo wake kijeshi na kijamii”.