Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chakusudia kufanya nadwa kwa njia ya mtandao kuhusu (kusihi kwa hadithi.. historia yake – usanifu wake).

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimekusudia kufanya nadwa ya kielimu kuhu (kusihi kwa hadithi.. historia yake – usanifu wake) kupitia program ya (zoom) siku ya Alkhamisi tarehe (16/07/2020m) saa kumi na moja jioni.

Mhadhiri wa nadwa hiyo atakuwa Ustadh Ahmadi Ali Majidi Alhilliy na itaongozwa na Sayyid Abdulhakim Swafi, nadwa hii ni sehemu ya harakati za kitengo hiki wakati huu ambao Atabatu Abbasiyya imechukua hatua za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Kwa maelezo zaidi piga simu kwa namba zifuatazo (07711173108).

Kumbuka kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kijamii ni moja ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinahusika na mambo ya kijamii na kusambaza fikra za Ahlulbait (a.s) kupitia idara zake mbalimbali zinazo wakilishwa na, Maahadi ya Quráni tawi la wavulana, Maahadi ya Quráni tawi la wasichana, kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Hilla, kituo cha turathi za Basra, shule za Dini za wasichana Alkafeel, idara ya habari na maarifa, hufanya harakati tofauti za mambo mbalimbali ya kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: