Asubuhi ya Jumanne ya mwezi (22 Dhulqaada 1441h) sawa na tarehe (14 Julai 2020m) waziri mkuu wa Iraq Sayyid Mustwafa Alkadhimi ametembelea shirika la Khairul-Juud ambalo lipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia utendaji wake katika sekta ya kilimo na viwanda, pamoja na mchango wake mkubwa katika kupambana na janga la Korona, kwa kutengeneza barakoa na vitakasa mikono bora kwa bei nafuu.
Waziri mkuu ametembelea sehemu mbalimbali za uzalishaji wa shirika hilo akiwa pamoja na wafanyakazi wa maeneo hayo, amesikiliza maelezo yao kuhusu utendaji kazi na uzalishaji wanaofanya.
Tumeongea na mkuu wa shirika la Khairul-Juud kuhusu ziara hiyo, amesema kuwa: “Ziara hii imemthibitishia waziri mkuu ubora wa bidhaa tunazo zalisha katika sekta ya kilimo na viwanda, pia ametambua kazi kubwa tunayo fanya katika kupambana na janga la Korona kwa kutengeneza barakoa na vitakasa mikono bora na kuviuza kwa bei rahisi ambayo kila mwananchi anaweza kuimudu”.
Akaongeza kuwa: “Tunatarajia Mheshimiwa waziri mkuu atatilia umuhimu mkubwa swala la uboreshaji wa sekta ya kilimo na viwanda”.