Waziri mkuu wa Iraq ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya leo mwezi (22 Dhulqaada 1441h) sawa na tarehe (14 Julai 2020m) waziri mkuu wa Iraq Sayyid Mustwafa Alkadhimi ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Amepokewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar na naibu wake pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, kisha akaenda kufanya ibada ya ziara na kuswali mbele ya kaburi takatifu la Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kuwa Mheshimiwa waziri mkuu wa Iraq Mustwafa Alkadhimi leo ametembelea mkoa mtukufu wa Karbala, miongoni mwa sehemu alizotembelea pia ni shirika la Khairul-Juud ambalo liko chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: