Kitengo cha usimamizi wa kihandisi: Kukamilika kwa hatua ya nne ya ujenzi wa kituo cha sita cha Alhayaat katika mkoa wa Muthanna

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamemaliza hatua ya nne katika ujenzi wa kituo cha sita cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kwenye mkoa wa Muthanna, wamemaliza kazi ya kufunga (Jipsam-Bord) pamoja na (Sandwich-Panel) kweye boma la juma kwa asilimia %100.

Mhandisi mkazi wa mradi Swafaa Muhammad Ali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kumaliza kujenga kuta kwa kutumia (Sandwich-Panel) kwenye boma la chuma, tulianza kufunga (Jipsam-Bord) kazi hiyo imekamilika pia”.

Akaongeza kuwa: “Kazi inaendelea vizuri kama ilivyo pangwa, tupo katika hatua nzuri, kazi zinazo endelea kwa sasa ni:

  • - Kazi ya kufunga madirisha (PVC).
  • - Kazi ya kuweka dari.
  • - Kazi ya kufunga (PVC) kwenye vyumba (114).
  • - Kuweka mfuma wa maji kwenye vyoo vya vyumbani.
  • - Kuweka mfumo wa zimamoto.
  • - Kuweka marumaru kwenye vyoo vya vyumbani, na kukamilisha mfumo wa vyoo vingine.
  • - Kufunga mfumo wa kuingiza hewa safi (AIR FRESH).
  • - Kuendelea kufunga nyaya za umeme.
  • - Kuweka lami na ruva kwenye maeneo ya uwazi na njia za kituo.
  • - Kuweka marumaru kwenye vyoo vyote (114) vya vyumbani.
  • - Tumemaliza kufuka (Jipsam-Bord) kwa asilimia %100.
  • - Tumemaliza kukata vyumba kwa asilimia %100.
  • - Kumaliza kujenga boma la chuma kwa asilimia %100.
  • - Kumaliza kujenga msingi kwa asilimia %100.

Kumbuka kuwa kituo hiki kinajengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kusaidia kupambana na janga la virusi vya Korona, na kuongeza uwezo wa hospitali ya Hussein (a.s) katika mkoa wa Muthanna, kwenye uwanja wenye ukubwa wa mita (3500), kina vyumba 114 vya wagonjwa, kinajengwa kwa kuzingatia matakwa ya wanufaika chini ya vigezo na kanuni za afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: