Idara ya uhusiano wa vyuo inajiandaa kufanya warsha kuhusu namna ya kufanya mtihani wa wanafunzi wa chuo kwa njia ya mtandao na imetoa wito wa kushiriki kwenye warsha hiyo

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano ya vyuo vikuu chini ya kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel imepanga kufanya warsha kwa njia ya mtandao, kuhusu namna ya kufanya mitihani ya wanachuo kwa mtandao (Google Classroom) na (Moodle), warsha hiyo inakusudia kufundisha mambo muhimu katika utumiaji wa program hizo ambazo zitatumika kufanya mitihani ya mwisho wa mwaka kwa wanachuo, kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, warsha itaanza kesho, siku ya Alkhamisi mwezi (24 Dhulqaada 1441h) sawa na tarehe (16 Julai 2020m), na itaendelea kwa muda wa siku mbili, kipindi cha saa moja kila siku kuanzia saa kumi na moja jioni hadi saa kumi na mbili.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Maahir Khalidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Warsha hiyo itafanywa kwa kutumia program ya (ZOOM) na mhadhiri atakuwa Ustadh Wasaam Ali Khuzaai, atazungumza kuhusu program mbili tulizo taja hapo awali, kwani zinatarajiwa kutumiwa na vyuo vingi kwenye mitihani yao ya mwisho wa mwaka”.

Akaongeza kuwa: “Watafundishwa namna ya kutumia program hizo kwenye warsha hii, ili kuwasaidia wanafunzi waweze kuzitumia kwa usahihi na kuwaepusha na makosa, ukizingatia kuwa ni jambo jipya linalo fanywa kwa mara ya kwanza kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa”.

Akasema kuwa: “Unaweza kushiriki kwenye warsha kwa kutumia link ifuatayo: (https://zoom.us/j/3765490911ID: 3765490911).

Pia masomo yatarushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook ufuatao: https://www.facebook.com/AlKafeel.Youths/ na kwenye youtube: https://www.youtube.com/channel/UCNVXTFY--WvLGUySyyMiCSg

Washiriki woto watapewa vyeti vya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: