Kikundi cha majibu ya haraka cha kujitolea katika kikosi cha Abbasi kimeanza kutoa huduma katika mji wa Bashiri

Maoni katika picha
Kikundi cha majibu ya haraka cha kujitolea chini ya kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) katika wilaya ya Bashiri mkoani Karkuuk, kimeanza kutoa huduma ya matibabu ya majumbani kwa wagonjwa wa Korona bure.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa huduma za matibabu zinatolewa kwa kuwasiliana na kitengo cha dharura cha idara ya afya ya mkoa wa Karkuuk, kinacho undwa na madaktari pamoja na wauguzi waliopata mafunzo maalum ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, sambamba na kufuata maelekezo ya viongozi wa kikosi cha Abbasi wa wilaya hiyo.

Aidha ni sehemu ya kufanyia kazi muongozo wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kufuata maelekezo ya idara ya afya, pia ni sehemu ya mkakati wa kikosi cha Abbasi katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona tangu kuripotiwa kwa virusi hivyo, kimekuwa kikipuliza dawa kwenye makazi ya watu ndani na nje ya mkoa wa Karbala, na kinafanya kila kiwezalo kupambana na janga hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: