Kitengo cha maendeleo endelevu kimemaliza semina ya maadili (Atiketi) kwa watumishi wa hospitali ya rufaa Alkafeel

Maoni katika picha
Kitengo cha maendeleo endelevu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimemaliza semina ya maadili (Atiketi) ya utumishi, iliyo totewa kwa watumishi wa hospitali ya rufaa Alkafeel mjini Karbala, kwa lengo la kuongeza uwezo wa kukabiliana na changamoto kazini.

Mkufunzi wa semina hiyo alikuwa ni Ustadh Ali Shimri, amesema kuwa: “Tumemaliza semina ya maadili (Atiketi) ya utumishi waliyo pewa baadhi ya watumishi wa hospitali ya rufaa Alkafeel, wamepewa semina hiyo baada ya uongozi wa hospitali kuomba watumishi wake wapewe semina”.

Akaongeza kuwa: “Tumeweka ratiba nzuri ya semina hiyo, tunakutana na watumishi pamoja na kutathmini mazingira ya ndani na nje ya hospitali, sambamba na kuweka mikakati ya kimaadili (Atiketi) kwa watumishi, inayo endana na wahudumu wa hospitali ili kutoa huduma bora kwa mgonjwa”.

Akasema: “Ratiba hiyo inavipengele vingi muhimu, ikiwa ni pamoja na kuamiliana na wagonjwa na wauguzi, pia jinsi ya kuamiliana na watu wenye umri mkubwa pamoja na vijana sambamba na kutengeneza mabalozi wa hospitali, na namna ya kuamiliana na mazingira tofauti na matumizi ya mitambo ya kisasa pamoja na mawasiliano ya mitandao ya kijamii”.

Kumbuka kuwa kitengo cha maendeleo endelevu kinajukumu la kutoa semina za kujenga uwezo wa watumishi wa Ataba kwenye sekta tofauti, kwa lengo la kuongeza uwezo na kuboresha utendaji wao, chini ya wakufunzi mahiri na wabobezi wa mambo mbalimbali ya maendeleo ya binaadamu kutoka ndani na nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: