Kwa upasuaji wa aina yake: kikosi cha madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel kimefanikiwa kumtibu kijana mwenye umri wa miaka ishirini aliyekuwa na tatizo la kuvunjika kwa mfupa

Maoni katika picha
Kikosi cha madaktari wa mifupa katika hospitali ya Alkafeel kimefanikiwa kumtibu kijana mwenye umri wa miaka ishirini aliyekuwa na tatizo la kuvunjika mfupa wa paja la kushoto zaidi ya mara moja.

Daktari bingwa wa mifupa katika hospitali hiyo, Dokta Ihsaan Faraji amesema kuwa: “Jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu limefanikiwa kumtibu mgonjwa mwenye umri wa miaka ishirini aliyekuwa na tatizo la kuvunjika mfupa wa paja la kushoto zaidi ya mara moja, tatizo lake lilikuwa kubwa kutokana na kufanyiwa upasuaji mara nyingi bila mafanikio kwenye hospitali zingine”.

Akaongeza kuwa: “Tumefanya upasuaji na kurekebisha mfupa wa paja, pamoja na kupandikiza kipande cha mfupa mpya ili kuwezesha goti kufanya kazi vizuri”.

Akabainisha kuwa: “Sehemu iliyovunjika tumeiwekea Shishi-Quful (kifaa cha kuunganishia mifupa)” akasema kuwa “Athari ya kuvunjika kwa mfupa ilikuwa inaonekana kwa nje jambo lililokuwa linasababisha ugumu wa kuunga kwa mfupa huo”.

Akasema: “Vifaa tiba vya kisasa vilivyopo katika hospitali vimesaidia sana kufanikisha kwa matibabu haya, mgonjwa ameweza kusimama kwa mguu wake kwa mara nyingine baada ya saa (24) tangu kufanyiwa upasuaji”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel huhakikisha inatoa huduma bora daima kwa vifaa tiba bora na vya kisasa chini ya madaktari mahiri wa kitaifa na kimataifa, jambo ambalo limeifanya kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali zingine za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti kila baada ya muda fulani, pamoja na kupokea wagonjwa wa aina zote waliopo katika hatua tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: