Mwezi (25) Dhulqaada ni siku ya kutandikwa ardhi na kusambaa kwa rehema ya Mwenyezi Mungu

Maoni katika picha
Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: (Na juu ya hivyo ameitandika ardhi) Naziaat: 30, ameitandika na kuifanywa kuwa mahala pa kuishi na kutembea, na katika kitabu cha (Muhawalatu lifahmi asriy lilqurán) neno “Dahaaha” maana yake: ardhi ameiumba kama yai, maana hiyo inakubaliana na mtazamo wa wana anga kuhusu umbo la ardhi.

Neno “Dahaa” linamaana ya kutandika pia, nalo ni neno pekee la kiarabu ambalo linamaana ya kutandika na duara kwa wakati mmoja, kwa hiyo katika hali ya awali ardhi inaonekana imetandikwa na uhalisia wake ipo katika umbo la duara.

Sehemu ya kwanza kuumbwa katika ardhi ni pale ilipo Kaaba takatifu, kisha Mwenyezi Mungu akapanua ardhi kutokea sehemu hiyo, na hiyo ndio maana ya kwamba alitandika ardhi kuanzia chini ya Kaaba takatifu.

Siku iliyo tandikwa ardhi:

Ardhi ilitandikwa mwezi ishirini na tano Dhulqaada, ni siku tukufu na imesuniwa kufunga, imepokewa kutoka kwa Imamu Mussa bun Jafari (a.s) anasema: (Mwezi ishirini na tano Dhulqaada Mwenyezi Mungu aliteremsha Kaaba nyumba takatifu, atakaefunga siku hiyo itakuwa ni kafara ya miaka sabini, nayo ndio siku ya kwanza aliyo teremsha rehema kwa Adam (a.s) kutoka mbinguni).

Kutoka kwa Muhammad bun Abdillahi Swaiqal, anasema: Alikuja kwetu Abul-Hassan –Ridhwa (a.s)- mwezi ishirini na tano Dhulqaada, akasema: (Fungeni mimi nimeamka na swaumu). Tukamuuliza funga gani? Akasema: (Siku iliyo shushwa rehema, ikatandikwa ardhi, ikasimamishwa Kaaba na akateremshwa Adam a.s).

Kutoka kwa Abdurahmaani Sullamiy, kutoka kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abuu Twalib (a.s) anasema: (Rehema ya kwanza kushushwa mbinguni kuja ardhini ilikuwa mwezi ishirini na tano Dhulqaada, atakaefunga mchana huo na akaswali usiku wake, ataandikiwa thawabu za kufanya ibada miaka mia moja sawa na kafunga mchana na kuswali usiku kwa muda huo).

Imetajwa katika baadhi ya vitabu vya dua kuwa miongoni mwa ibada iliyo suniwa siku ya kutandikwa ardhi, ni kumzuri Imamu Ridhwa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: