Baada ya kufanikiwa awamu ya kwanza: Kituo cha utamaduni wa familia kimeanza awamu ya pili ya ratiba ya (Kitabu changu thamani yangu)

Maoni katika picha
Kitengo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza awamu ya pili ya ratiba ya (kitabu changu thamani yangu) inayo husisha wasichana wa kila umri kwa lengo la kuongeza maarifa kwa wanawake na kutumia wakati wao wa faragha kwa mambo yenye manufaa kwao, hii inatokana na mafanikio makubwa yaliyo patikana katika awamu ya kwanza pamoja na ukubwa wa idadi ya washiriki na shauku yao ya kutaka kushiriki kwa mara ya pili.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo hicho Ustadhat Asmahani Ibrahim, amesema kuwa: “Ratiba ya mara ya kwanza ililenga kuangalia namna program itakavyo kubaliwa na washiriki, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tulifanikiwa kupata tulicho kusudia, ndio sababu ya kuandaa awamu ya pili kwa lengo la kuhuisha utamaduni na kujitambua, pamoja na kutumia muda kwa mambo yenye faida”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba hii itatoa maswali kwa njia ya mtandao, yatakayo lenga kutambua uwezo wa washiriki na hali ya maisha yao ya kila siku, baada ya kusoma kitabu kilicho pangwa kisemacho (Kujenga shakhsiyya baina ya ukweli na uongo), unaweza kupakua kitabu hicho kupitia link ifuatayo: https://drive.google.com/file/d/1LTXiifBCYxtn2ljZVAgQ4vw_zuAZ0O0v/view

Na utaweza kushiriki kwa kutumia link ifuatayo: https://forms.gle/rQViAaAbfBqiBuHRA

muda uliopangwa ni siku kumi na tano za kusoma na kufanya mtihani, kuna zawadi za washindi watatu kwa mwanzo watakao patikana baada ya kupiga kura”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: