Kamati ya maelekezo na misaada inaendelea kusiliana familia za wahanga na imewapa zaidi ya vifurushi 2500 vya chakula

Maoni katika picha
Kamati ya maelekezo na misaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na taasisi ya Answaaru-Zaharaa (a.s) Alkhairiyya, inaendelea kusaidia familia za wahanga wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, chini ya program ya (Marjaiyyatu-Takaaful) iliyo anzishwa na Ataba tukufu katika kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu, wamefanikiwa kugawa zaidi ya vifurushi 2500 vya chakula katika mitaa ya Karbala chini ya utaratibu maalum ulio pangwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kamati hiyo Shekh Haidari Aáridhi, akaongeza kusema kuwa: “Katika kuitikia wito wa kusaidiana ulio tolewa na Marjaa Dini mkuu, tumeandaa na kugawa vifurushi hivyo vya chakula kwa familia za watu wenye kipato kidogo na mafakiri katika mkoa mtukufu wa Karbala”.

Akafafanua kuwa: “Tumegawa vifurushi vilivyokuwa na aina tofauti za nafaka za chakula na tutajitahidi kufikia familia nyingi zaidi chini ya utaratibu uliopangwa, pamoja na kuendeleza program zingine”.

Kumbuka kuwa Marjaa Dini mkuu alitoa wito wa kuunganisha ngugu katika kuzihudumia familia za watu wenye kipato kidogo na mafakiri walio athiriwa na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ndipo Ataba tukufu ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) kwa ajili ya kusaidia familia za wahanga hao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: