Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mradi huu unatekelezwa na shirika la ardhi takatifu la Iraq chini ya usimamizi wa kitengo chetu, ni miongoni mwa miradi muhimu, umeanza baada ya kumaliza uwekaji wa marumaru katika uwanja wa haram pamoja na kazi zingine, nao utakamilisha sehemu muhimu ya ujenzi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa: “Tumeanza na mlango wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s), kazi hii itakuwa na vipengele vifuatavyo:
- - Kuandaa taarifa maalum ya kila mlango, ambapo kuna jumla ya milango tisa, taarifa hizo ziendane kiujenzi na muonekano wa nje wa mlango husika pamoja na muonekano wa ndani ya haram tukufu.
- - Kuondoa mabaki ya jengo la zamani.
- - Kufunga nyaya za umeme kwenye mifumo yote ya kutoa huduma na kuiunganisha na mifumo mingine ndani ya haram tukufu, kama vile kamera, mawasiliano, mfumo wa kutoa onyo na mingineyo.
- - Kufanya matengenezo rasmi kwenye kila mlango kwa kutumia vifaa maalum.
- - Kuweka Kashi-Karbalai na kuongeza nakshi na mapambo.
- - Kuweka kipande cha mlango wa zamani kwa ndani bila kuonekana upande wa nje.
- - Kuweka marumaru maalum kwenye sakafu za milangoni”.
Akasisitiza kuwa: “Baada ya kumaliza kazi hii makundi ya watu yatapita vizuri bila msongamano hususan wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu”.
Tambua kuwa mradi wa upanuzi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umekuwa na miradi mingi ya ujenzi ambayo yote kwa ujumla ni sehemu ya mradi huo mkubwa, uliokuwa haujafanywa kwa karne nyingi, miongoni mwa miradi hiyo ni huu wa kupanua milango mikuu ya haram tukufu.