Kituo cha taaluma za namba kinafanya mkutano kwa njia ya mtandao na wawakilishi wa chuo kikuu cha Mosul kwa lengo la kutambulisha miradi ya kituo

Maoni katika picha
Katika uwanja wa kusaidiana kielimu kati ya Atabatu Abbasiyya na vyuo pamoja na taasisi za kielimu za Iraq, kituo cha taaluma za namba chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Ataba tukufu wamefanya mkutano kwa njia ya mtandao na wawakilishi wa chuo kikuu cha Mosul, akiwemo katibu mkuu wa chuo cha Mosol Ustadh Sefu Ashiqar.

Mkutano ulikuwa unahusu mambo mawili makuu, kwanza kuonyesha fikra na malengo ya mradi wa namba hapa Iraq katika elimu ya vyuo, nao ni mradi wa kutoa huduma sio wa kutengeneza faida, umejikita katika kukusanya maoni na kazi za wanachuo kwa njia ya mtandao, kwenye masomo yote ya vyuo vya Iraq, na jambo la pili lilikuwa linahusu kuhifadhi matokeo ya tafiti za kielimu yanayo weza kufanyiwa kazi kimtandao na kulinda yasiharibike au kuibiwa.

Mwishoni wakajadili ushirikiano baina ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya na kituo cha taaluma za namba pamoja na maktaba kuu ya chuo cha Mosul sambamba na kujiunga kwake kwenye miradi hii miwili kutokana na maendeleo ya teknolejia, tumekubaliana kuendeleza ushirikiano kwa ajili ya kufikia lengo la shirika kwa maslahi ya jamii ya raia wa Iraq.

Tambua kuwa lengo la kuanzishwa miradi hii ni kutunza kazi za wanafunzi wa chuo na kurahisisha matumizi ya kazi hizo, pamoja na kuzipa umuhimu unao takiwa kazi za kielimu zinazo fanywa na wanafunzi pamoja na walimu.

Kumbuka kuwa kituo cha taaluma za namba kinatoa huduma bure kupitia miradi miwili tuliotaja, kwa kila anayependa kuchangia katika kutunza matokeo ya elimu kitaifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: