Kituo cha sita katika mkoa wa Muthanna kimekamilika kwa asilimia %85 na kitaanza kufanya kazi hivi karibuni

Maoni katika picha
Ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona Alhayaat cha sita, kinacho jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkoa wa Muthanna kimekamilika kwa asilimia %85, kituo hicho ni sehemu ya mfululizo wa miradi inayo tekelezwa na Ataba tukufu kwenye mikoa tofauti ya Iraq, kupitia kitengo chake cha usimamizi wa kihandisi.

Mradi huu ni sehemu ya kuisaidia wizara ya afya katika kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona na kupunguza msongamano wa wagonjwa hao mahospitalini sambamba na kuhakikisha wanapata huduma bora za afya.

Kiongozi wa idara ya tiba katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Osama Abdul-Hassan amesema kuwa: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi tunafanya ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha sita katika mkoa wa Muthanna, kwa ufadhili wa wizara ya afya na mkoa wa Muthanna pamoja na jopo la wahisani, watendaji wa mradi huo ni kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Ujenzi wa kituo hicho umefika zaidi ya asilimia (%85), kituo hiki kitakuwa na vitanda vya wagonjwa zaidi ya mia moja, kinatarajiwa kuanza kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona hivi karibuni Insha-Allah”.

Kumbuka kuwa ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha sita katika mkoa wa Muthanna, ni sehemu ya vituo vitatu vinavyo jengwa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkoa wa Bagdad na Baabil, aidha ni sehemu ya vituo vinne vilivyo jengwa hapo awali, viwili katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu, na kimoja katika hospitali ya Hindiyya mkoani Karbala, huku kituo cha nne kikijengwa kwa ufadhili ya hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu, vituo vyote vimetokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na muongozo wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi wa kusaidia wahudumu wa afya kupambana na janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: