Arshu-Tilawah inaendelea na harakati zake za matangazo mubashara

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni chini ya Maahadi ya Quráni katika Ataba tukufu kinaendelea na harakati zake za vikao vya usomaji wa Quráni kila wiki ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kupitia matangazo mubashara.

Usomaji huo unafuata taratibu zote za kujikinga na maambukizi pamoja na kujiepusha na mkusanyiko, kisomo hicho kinarushwa na luninga ya Karbala pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii.

Kisomo kitukufu kinafanywa na wasomi mahiri wa Atabatu Abbasiyya.

Tambua kuwa mradi wa Arshu-Tilawah unalenga kunufaika na vipaji vya usomaji wa Quráni vilivyopo Iraq, na kuvionyesha katika ulimwengu wa kiislamu, sambamba na kuviendeleza chini ya utaratibu maalum unaosimamiwa na walimu walio bobea katika fani hiyo, mradi huu umeshapiga hatua kubwa na wasomi wengi wamesha shiriki, mradi huu ulisimama baada ya kuingia janga la Korona, sasa unarudi tena kwa mara nyingine katika mazingira ya kufuata tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, imezowea kufanya harakati mbalimbali zinazo husu Quráni kila mwaka, lakini kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa pamoja na hatua zilizo chukuliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu za kujikinga na maambukizi ya janga hili, mwaka huu tumetosheka na mambo machache.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: