Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram wamemaliza kazi ya kusafisha kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya wamemaliza kazi ya kusafisha kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) nje na ndani.

Tumeongea na makamo rais wa kitengo cha usimamizi wa haram Sayyid Zainul-Aabidina Adnani Quraishi amesema kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu husafisha Kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kila baada ya muda fulani, husafisha kati ya mara tatu hadi mara nne kwa mwaka, kazi hiyo hufanywa kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya kusafisha kubba hugawanywa katika hatua tofauti na hudumu kwa zaidi ya siku moja, kubba husafishwa nje na ndani, hutumiwa vifaa maalum vya kusafishia visivyo haribu dhahabu iliyopo kwenye kubba hilo, na vinavyo saidia kuilinda isiharibike kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, aidha hutumika pia kitambaa cha pamba kukausha vifuniko vya dhahabu baada ya kumaliza kuviosha”.

Akaendelea kusema: “Hatutumii aina yeyote ya kemekali, tunatumia maji masafi peke yake”.

Akafafanua kuwa: “Watumishi wanaopewa nafasi ya kufanya kazi hiyo ni wale waliopewa mafunzo maalum ya uoshaji wa kubba hilo kutokana na umakini mkubwa unaotakiwa katika kazi hiyo”.

Tambua kuwa kitengo cha usimamizi wa haram kina majukumu mengi katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile kufagia, kupiga deki, kutandika miswala na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: