Maombolezo ya kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s)

Maoni katika picha
Wapenzi na wafuasi wa maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika siku kama hizi za mwisho wa mwezi wa Dhulqaada, huomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) aliye uwawa mwaka wa (220h).

Imamu Muhammad bun Ali Aljawaad (a.s) ni Imamu wa tisa katika Maimamu wa Ahlulbaiti walio husiwa na Mtume (s.a.w.w) –kwa amri wa Mwenyezi Mungu mtukufu- waliochukua madaraka ya uimamu baada yake na baada ya Quráni kuthibitisha utakasifu wao.

Riwaya zinaonyesha kuwa Mu’taswimu Abbasi alijaribu mara nyingi kumuua Imamu Aljawaad (a.s), na mwishoni akaamua kumtumia Ummul-Fadhil kutekeleza jinai yake.

Jafari bun Ma-Amun akawasiliana na dada yake (Ummul-Fadhil) mke wa Imamu Aljawaad (a.s), Ummul-Fadhil hakua na tabia nzuri, Jafari alikua anajua wivu aliokua nao kwa mke mwingine wa Imamu (mama wa Imamu Al-Haadi), akamshawishi amuue mme wake na akamuonyesha namna ya kumuua, Ummul-Fadhil akakubali, Jafari akampa sumu kali aliyopewa na Mu’taswim, naye Ummul-Fadhil amakuwekea Imamu kwenye chakula, inasemekana alimuwekea kwenye zabibu alizokuwa akizipenda sana Imamu, baada ya kula Imamu alisikia maumivu makali na akaanza kutapika damu, akalala kitandani na akaanza kugeuka kulia na kushoto, hadi akatapika ini ndipo akafariki Imamu wetu kipenzi (a.s) akiwa ni shahidi mdhulimiwa, sauti za vilio zikasikika katika nyumba yake, familia na wafuasi wake walilia na kuhuzunika sana, wakawa wanaita: Ewe Imamu wangu.. Ewe Jawaad.. Ewe msaidiaji wa mayatima na masikini.. Ewe kimbilio la walio potea na wenye shida.. Imamu akawa amekwenda kwenye makazi yake ya milele, na mtoto wake Imamu Ali Alhaadi akamuandaa, akamuosha na kumvisha sanda kisha akamzika pembezoni mwa kaburi la babu yake Imamu Mussa Alkadhim (a.s), alifariki mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaada mwaka wa (220h) akiwa bado kijana mdogo, nyota ya uongofu na uchamungu ikazimika, ukurasa wake wa maisha ukafungwa.

Amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa (a.s) na siku aliyo uwawa na siku atakayo fufuliwa na kutoa ushahidi kwa umma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: