Mazingira ya huzuni yameenea katika eneo lote la Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na kumbukumbu ya kifo cha Imamu Jawaad (a.s), aliye fariki mwishoni mwa mwezi wa Dhulqaada mwaka wa 220 hijiriyya, ni majonzi na huzuni kubwa kuondokewa na mwezi wa tisa miongoni mwa miezi ya Muhammadiyya na Imamu Mungofu, tawi tukufu la mti mtakatifu unaotoa matunda wakati wote kwa idhini ya Mola wake, ni Imamu aliyesomesha wanachuoni wakubwa akiwa na umri mdogo, kwa nini asiwe hivyo wakati yeye ni katika watu wa nyumba ya Mtume chemchem ya elimu, babu yake ni Mtume Muhammad na Ali na mama yake ni Fatuma Zaharaa (a.s).
Kuta za haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imefunikwa vitambaa vyeusi kuashiria huzuni kwa kuondokewa na Imamu kielelezo cha ubinaadamu.
Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba kamili ya kuomboleza msiba huu, yenye vipengele vichache kulingana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa kutokana na janga la Korona, sambamba na maelekezo ya idara ya afya yanayo kataza mikusanyiko ya watu, kitengo cha dini kimeomboleza msiba huu kwa kutoa muhadhara chini ya uhadhiri wa Sayyid Adnani Mussawi, amezungumzia historia ya Imamu huyo na mchango wake kwa umma wa kiislamu na kibinaadamu kwa ujumla, hususan katika sekta ya elimu ambayo alisifika nayo tangu akiwa mdogo.