Mwezi mosi Dhulhijjah ni siku ya kumbukumbu ya ndoa ya nuru kwa nuru

Maoni katika picha
Mwezi mosi Dhulhijjah mwaka wa pili hijiriyya ilifungwa ndoa takatifu baina ya Imamu Ali na Fatuma Zaharaa (a.s) ambayo iliitwa ndoa ya nuru mbili.

Tukio hilo linaumuhimu mkubwa katika historia kwa sababu hao ni watu bora baada ya Mtume (s.a.w.w), na matunda ya ndoa hiyo ni kupatikana kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s) hali kadhalika ndoa hiyo inaonyesha nafasi ya Imamu Ali (a.s) mbele ya Mtume (s.a.w.w) kwa kumuozesha mtoto wake.

Kitabu cha Kashfu-Ghummah kimeandika kuwa, maswahaba wengi walikwenda kumposa bibi Fatuma (a.s) lakini Mtume (s.a.w.w) alikataa, alipo kwenda kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) alifurahi sana na akasema: (Hakuna mtu anaemfaa Fatuma zaidi ya Ali).

Kwa mahari ndogo na harusi ya kawaida chini ya amri ya Mwenyezi Mungu, ndoa ya nuru kwa nuru ikakamilika, bibi Fatuma Zaharaa akaolewa na Ali bun Abu Twalib (a.s) wakawa kituo cha nuru inayo angazia ulimwengu kwa nuru ya uislamu na Quráni, baada ya kukamilika Dini chini ya usimamizi wa Mtume (s.a.w.w), na ikatimia neema kwa waislamu, Mwenyezi Mungu akaridhia uislamu kuwa Dini ya walimwengu.

Kutoka kwa Khabaab bun Arti anasema: Mwenyezi Mungu mtukufu alimuambia Jibrilu kuwa Nuru imeolewa na Nuru, Walii alikuwa ni Mwenyezi Mungu, na mposaji Jibrilu, mualikaji Mikaeli, muitaji Israfiil, mhudumiaji Izraeel, mashahidi walikuwa ni malaika wa mbinguni na ardhini, kisha akauambia mti wa Toba utoe matunda yake, ukatoa Duru nyeupe na Yakuti nyekundu na Zabrajadi za kijani na Lulu.

Ulipofika usiku wa harusi Mtume alikuja na farasi wake, akamuambia Fatuma: Panda, Akamuambia Salmani amuongoze huku mtume (s.a.w.w) akumuendesha, alipokuwa njiani Mtume (s.a.w.w) akasikia sauti ya msafara wa Jibrilu akiwa na malaika elfu sabini, na Mikaeli akiwa na malaika elfu sabini, Mtume (s.a.w.w) akawauliza: mmekuja kufanya nini ardhini? Wakasema: tumekuja kumshindikiza Fatuma kwa Ali bun Abu Twalib, Jibrilu akasoma takbira na Mikaeli akasoma takbira, malaika wakasoma takbira na Mtume Muhammad akasoma takbira, maharusi wakasomewa takbira katika usiku huo.

Matunda ya ndoa hiyo tukufu yalikuwa ni watoto watano, ambao ni maimamu wawili watakasifu Hassan Almujtaba na bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s), na wanawake wawili ambao ni Aqilah bani Hashim Zainabu Alkubra na Ummu-Kulthum (a.s), walizaliwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w), mtoto wa mwisho alikuwa ni Muhsin (a.s) ambae mimba yake ilitoka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: